AWITI NJE
- DERRICK INGARA

- Feb 20, 2018
- 1 min read

Cyprian Awiti during a past event. Photo|Nation media
Gavana wa Homabay Cyprian Awiti amepata pigo baada ya ushindi wake kutupiliwa mbali. Mahakama kuu ya Homabay imeamua kuwa uchaguzi uulikumbwa na visa vya udanganyifu mnamo Agosti Nane. Jaji Joseph Karanja ameamua kuwa tume ya IEBC ilifeli kuandaa uchaguzi huru na wazi Agosti nane mwaka jana.
Kesi hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa mbunge wa Kasipul Oyugi Magwanga. Awiti amekuwa gavana wa pili kupoteza kiti mwaka huu baada ya Mohamed Abdi wa Wajir mwezi uliopita. Polisi wamefyatua risasi kuwatawanya wafuasi wa wanasiasa hao waliokuwa wamekusanyika mahakakani.
Uchaguzi mpya unatarajiwa kuandaliwa katika eneo iliwakaazi hao wapate gavana mpya.























Comments